Testimonies
Kampuni ya TiME TICKETS, leo imezindua rasmi mfumo wa kisasa wa uchangishaji pesa unaotambulika kwa jina la WEZESHAsasa. Mfumo huu wa kwanza kubuniwa kwenye historia ya uendeshaji wa uchangiaji wa hiyari (Harambee) Tanzania, unayahakikishia mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kirai, vikundi, idara za serikali na taasisi za kidini kuwa, hivi sasa kazi zote za uratibu wa michango ya hiyari zinaenda kufanyika kwa uwazi na ufanisi wa hali ya juu.
“Wananchi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni waungwana pia ni wepesi wa kujitoa kwa kuchangia katika shughuli za kijamii na kiuchumi wakilenga kujiletea maendeleo. Sio jambo la kustaajabisha kuona Watanzania wakisimama kwa pamoja kuchangia jamii zilizoathiriwa na majanga mbali mbali kama mafuriko, moto, njaa, tetemeko nk. Hivyo basi, kushirikiana katika vipindi vigumu ni sehemu ya utamaduni wa Watanzania. Kampuni yetu imelitambua hilo na sasa tumebuni mfumo madhubuti unaolenga kukidhi mahitaji ya shughuli zote za uchangiaji wa hiyari katika jamii yetu” Amesema Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya TiME TICKETS, Josephat Mandara
Upatikanaji na Matumizi
Mfumo wa WEZESHAsasa unalenga kuleta mapinduzi makubwa ya matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano sambamba na kuimarika kwa utamaduni wa Watanzania kupenda kuchangia maendeleo yao wenyewe kama ilivyo kwenye nchi zingine zilizoendelea. Mfumo huu unaotumia TEHAMA unampa fursa kila mtu kuweza kuchangia kupitia moja kati ya njia hizi; tovuti (www.wezeshasasa.com), simu za kiganjani za androidi au ujumbe mfupi kwa wale wanaotumia simu za kawaida.
Urahisi wa Matumizi na Usalama wa Michango
“Dira ya maendeleo ya Tanzania inawaelekeza wananchi wake kuwa wameondokana na umaskini uliokithiri na kuufikia uchumi wa kati mara ifikapo 2025. Dhamira hii inatoa msukumo kwa Watanzania kuongeza bidii ya kujileta maendeleo na kufanya kazi zenye tija. Sisi kama taifa hatuwezi kuwa na dira na maono yanayokidhi mahitaji yetu na bado tukaendelea kuwa wategemezi wa misaada ya nje. Mfumo huu wa WEZESHAsasa umebuniwa kwa wakati muafaka kwani unaenda kungeza viwango vya kujitegemea, uwajibikaji, utawala bora na kuimarisha umoja katika kufikia dira ya maendeleo ya taifa letu…” Amesema mshauri elekezi wa kampuni ya TiME TICKETS, Avit Buchwa.
Ofisa Mkuu wa Ufundi na Teknologia wa TiME Tickets, Bw. Godluck Akyoo pia alieleza kuwa mfumo wa uchangiaji wa hiyari wa WEZESHAsasa ni rahisi sana kutumia kwani unayo namba moja tu ya kutuma pesa ambayo hutumika kupitia makampuni yote ya simu. Kwa mteja atakayepewa huduma ya WEZESHAsasa anahakikishiwa usalama wa hali ya juu wa pesa zake kwani wakati wote wa uchangiaji anaweza kuona hatua zote za mchakato wa pesa zinavyoingia kwenye akauti na anamuona kila mchanigiaji na kiwango alichotoa. Kampuni ya TiME TICKETS ambayo ni wamiliki wa mfumo wa WEZESHAsasa wanatoa ushauri wa kiufundi kwa kutumia namba maalum isiyokuwa na malipo kwa muda wa masaa 24/7.
Uwazi na Uwajibikaji
“ Mfumo wa WEZESHAsasa ni shirikishi kwani unatoa fursa kwa mratibu wa zoezi la uchangiaji wa hiyari na kila mchangiaji mahala popote aliko kuweza kuona taarifa zote za msingi za harambee husika. Mchangiaji anaweza kuipata huduma hii kupitia mtandao wa intaneti kwenye kompyuta au simu ya kiganjani. Uwazi mkubwa tuliouweka katika ubunifu huu unawafanya wachangiaji kuongeza imani kwa taasisi inayo ratibu harambee na hamasa ya kutaka kuendelea kuchangia zaidi ” Amesema Mkurugenzi wa Masoko TiME TICKETS, Mwasapi Kihongosi ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa WEZESHAsasa.
Kuhusu Kampuni ya TiME TICKETS
TiME TICKETS ni kampuni iliyoanzishwa nchini Tanzania na inasimamiwa na vijana wazawa wenye nia ya dhati kabisa ya kutoa majibu ya changamoto mbali mbali zenye kuzorotesha ukuwaji wa ustawi na maendeleo ya Watanzania hususani mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa fedha. TiME TICKETS ni kampuni iliyobobea katika masuala TEHAMA na ni zao la miradi inayoratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia kupitia mradi wa Dar es Salaam Technohama Bussiness Incubator (DTBi). Ofisi kuu ya TiME Tickets ipo jengo la COSTECH, Kijitonyama barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Kwa maelezo zaidi tembelea www.timetickets.co.tz
Kufahamu maelezo zaidi ya mfumo wa WEZESHAsasa, tafadhali tembelea www.wezeshasasa.com. Kwa maulizo na msaada zaidi tuandikie kupitia taarifa@wezeshasasa.com au piga simu 0752030032
— Godluck Akyoo 01 Jan, 1970 12:00 AM
Leo tarehe 19.5.2017 taasisi za TiME Tickets, Eco Valley Advisers, na Clouds Media wamekabidhi kwa uongozi wa mkoa wa Arusha waliopokea kwa niaba ya wafiwa, kiasi cha shilingi 4,444,031/- ikiwa ni rambi rambi zilizochangwa na watanzania kupitia mfumo wa harambee wa WEZESHAsasa (www.wezeshasasa.com). Fedha hizo zimepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo.
“Kama ilivo desturi ya Watanzania kuitikia kwa vitendo kusaidia kwa hali na mali pindi mtu, kikundi au jamii inapopatwa na majanga yasiyotarajiwa, taasisi za Clouds Media, Eco Valley Advisers na TiME Tickets walikubaliana kwa pamoja na kwa dhati kuunganisha nguvu za Watanzania wote pasipo kujali dini, hali, itikadi, jinsi na maeneo ya kijiografia wakiwa na dhamira ya kuhamasisha rambi rambi kwa takribani siku 4 ( 8 – 11 Mei 2017)” Alisema mkurugenzi wa TiME Tickets, Bwana Josephat Mandara.
Ndani ya kipindi hicho kifupi kisichozidi siku nne, wachangiaji wapatao 721 (huku watu 10 wakichanga zaidi ya mara moja, kufanya michango 731) waliweza kuchangia kiasi cha pesa za Kitanzania zipatazo shilingi 4,444,031/-. Wachangiaji wote na kiasi cha machango cha kila mmoja yanaweza kupatikana hapa. Jambo la kuzingatia na ambalo ni faraja kwa wote walioratibu zoezi hili sio wingi wa pesa wala idadi ya wachangiaji bali ni uwezo wa mfumo kuweza kuwaleta pamoja Watanzania wote. Sura pana ya utaifa inajidhihirisha kwenye aina ya michango. Kwa mujibu wa mtiririko wa uchangiaji, michango iliyopatikana ni kati ya shilingi 10/- hadi shilingi 700,000/- Tafsiri ya aina hii ya uchangiaji ni kwamba mfumo umeweza kuimarisha mshikamano wa Watanzania. Idadi hii ya watu na kiwango cha pesa vimepatikana kwa uwazi kama inavyoonekana katika tovuti. www.wezeshasasa.com/lucky
Kwa kuzingatia malengo ya ukusanyaji wa rambi rambi kama yalivokuwa yameainishwa kwenye tovuti, kila familia ya wafiwa itapokea kiasi cha shilingi 126,972/- Katika makabidhiano hayo mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo alisema “ Kwa niaba ya wafiwa na wananchi wa Arusha tumefarijika sana kuona kwamba Watanzania kwa umoja wao wamekuwa nasi katika kipindi hiki cha majonzi. Ni jambo la kutia moyo na kujivunia kwamba sasa upo mfumo wa harambee wa TEHAMA na ubunifu ambao unaweza kukusanya michango kwa ufanisi na uwazi”.
Makabidhiano ya rambi rambi yalifanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kushudiwa na Katibu Tawala wa mkoa Bw. Richard N. Kavitega, uongozi wa Shule ya Lucky Vincent na waadishi wa habari.
Unaweza kupata nakala ya taarifa ya makabidhiano (press release) hapa.
Kuona wachangiaji wote na kiasi chao walichotoa pakua dokumenti hii.
— Mwasapi Kihongosi 01 Jan, 1970 12:00 AM
We are truly grateful for joining hands with us in touching and transforming life of this pretty angel...she's back all tall and healthy...thanks for standing tall with her thanks for creating that smile be blessed abundantly tunawapenda sana.
You can check her campaign page here: https://wezeshasasa.com/jamila and read more about her story here: http://starlocalmedia.com/planocourier/the-taller-tanzanian-plano-hospital-offers-teen-girl-a-chance/article_1bf5ea40-a94f-11e7-b5dc-bf028751b06b.html
— Mwasapi Kihongosi 25 Nov, 2017 12:39 PM