WEZESHAsasa - Jukwa la Harambee

Je unahitaji kufanya harambee kwaajili ya mradi/ bidhaa au shughuli ya kimaendeleo? Tembelea sasa www.wezeshasasa.com kuanzisha harambee yako sasa! Je unahitaji msaada zaidi?
Wasiliana nasi kupitia taarifa@wezeshasasa.com au tupigie +255 752 030 032

 

Kuna gharama gani kuendesha harambee kupitia WEZESHAsasa?

Karibu WEZESHAsasa, na tunatarajia kampeni yako itakuwa yenye mafanikio. Hakuna gharama yeyote kufungua harambee yako kupitia jukwaa la WEZESHAsasa. Ili kusadia shughuli za uendeshaji wa mfumo huu, kuna tozo dogo linalokatwa kutoka jumla ya makusanyo yote. Tozo hili pekee la lazima la WEZESHAsasa ni 5% tu ya makusanyo yako yote, na hukatwa wakati wa mchangshaji anapochukua pesa zake. Kisha baada ya makato hayo, pesa baki hutumwa kwenda kwenye akaunti ya benki elekezi ya mchangishaji husika.

 

Huduma gani inatolewa kwa tozo hili la 5% ya makusanyo yote?

Kwa tozo hili la 5% mfumo wa WEZESHAsasa unakupa huduma ifuatayo:

  1. Ukurasa maalumu wenye kuelezea nia ya harambee yako pamoja na kutoa taatifa muhimu za michango kama jumla ya pesa iliyokusanywa, kikomo cha uchangiaji, kiasi kinachohitajika, taarifa/ mawasiliano ya mchangishaji, washirika wa mchangishaji
  2. Namba maalumu na ya kipekee ya kupokea michango kupitia mitandao ya simu TiGO Pesa, Airtel Money, MPESA.
  3. Kiuongo maalumu cha mtandao chenye jina maalumu na la kipekee kwaajili ya kurahisisha usambazaji habari
  4. Uwezo wa kupokea michango kupitia kutoka kwa watu mbalimbali kupitia namba maalumu.
  5. Kuona taarifa muhumu za michango kadiri inavyoendelea kuchangwa mubashara, muda wowote na mahali popote kupitia sehemu maalumu ya tovuti ya WEZESHAsasa.com
  6. Uwezo wa kutengeneza na kupakua ripoti maalumu ya michango, huku ukipata taarifa maalumu kama majina ya wachangiaji, mitandao waliyotumia kuchangia, muda na siku walizochanga nk.
  7. Sehemu maalumu ya kupokea maoni kutoka kwa wachangiaji
  8. Sehemu maalumu ya kutoa maendeleo/ taarifa muhimu kuhusu mchango harambee yako au utekelezaji wa nia ya mchango. Hii huongeza 

 

Je, kuna huduma na tozo zingine za ziada mbali na 5%?

Ndiyo. Tozo na huduma hizi si za lamima.