Mfumo wa kwanza wa harambee Tanzania wazinduliwa


Uzinduzi rasmi WEZESHAsasa mfumo wa uchangiaji kwa njia ya mtandao

Kampuni ya TiME TICKETS, leo imezindua rasmi mfumo wa kisasa wa uchangishaji pesa unaotambulika kwa jina la WEZESHAsasa. Mfumo huu wa kwanza kubuniwa kwenye historia ya uendeshaji wa uchangiaji wa hiyari (Harambee) Tanzania, unayahakikishia mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kirai, vikundi, idara za serikali na taasisi za kidini  kuwa, hivi sasa kazi zote za uratibu wa michango ya hiyari zinaenda kufanyika kwa uwazi na  ufanisi wa hali ya juu.

“Wananchi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni waungwana pia ni wepesi wa kujitoa kwa kuchangia katika shughuli za kijamii na kiuchumi wakilenga kujiletea maendeleo. Sio jambo la kustaajabisha kuona Watanzania wakisimama kwa pamoja kuchangia jamii zilizoathiriwa na majanga mbali mbali kama mafuriko, moto, njaa, tetemeko nk. Hivyo basi, kushirikiana katika vipindi vigumu ni sehemu ya utamaduni wa Watanzania. Kampuni yetu imelitambua hilo na sasa tumebuni mfumo madhubuti unaolenga kukidhi mahitaji ya shughuli zote za uchangiaji wa hiyari katika jamii yetu” Amesema Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya TiME TICKETS, Josephat Mandara

 

Upatikanaji na Matumizi

Mfumo wa WEZESHAsasa unalenga kuleta mapinduzi makubwa ya matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano sambamba na kuimarika kwa utamaduni wa Watanzania kupenda kuchangia maendeleo yao wenyewe kama ilivyo kwenye nchi zingine zilizoendelea. Mfumo huu unaotumia TEHAMA unampa fursa kila mtu kuweza kuchangia kupitia moja kati ya njia hizi; tovuti (www.wezeshasasa.com), simu za kiganjani za androidi au ujumbe mfupi kwa wale wanaotumia  simu za kawaida.

Urahisi wa Matumizi na Usalama wa Michango

“Dira ya maendeleo ya Tanzania inawaelekeza wananchi wake kuwa wameondokana na umaskini uliokithiri na kuufikia uchumi wa kati mara ifikapo 2025. Dhamira hii inatoa msukumo kwa Watanzania kuongeza bidii ya kujileta maendeleo na kufanya kazi zenye tija. Sisi kama taifa hatuwezi kuwa na dira na maono yanayokidhi mahitaji yetu na bado tukaendelea kuwa wategemezi wa misaada ya nje. Mfumo huu wa WEZESHAsasa umebuniwa kwa wakati muafaka kwani unaenda kungeza viwango vya kujitegemea, uwajibikaji, utawala bora na kuimarisha umoja   katika kufikia dira ya maendeleo ya taifa letu…” Amesema mshauri elekezi wa kampuni ya TiME TICKETS, Avit Buchwa.

Ofisa Mkuu wa Ufundi na Teknologia wa TiME Tickets, Bw. Godluck Akyoo pia alieleza kuwa mfumo wa uchangiaji wa hiyari wa WEZESHAsasa ni rahisi sana kutumia kwani unayo namba moja tu ya kutuma pesa ambayo hutumika kupitia makampuni yote ya simu. Kwa mteja atakayepewa huduma ya WEZESHAsasa  anahakikishiwa usalama wa hali ya juu wa pesa zake  kwani wakati wote wa uchangiaji anaweza kuona hatua zote za mchakato wa pesa zinavyoingia kwenye akauti na anamuona kila mchanigiaji na kiwango alichotoa. Kampuni ya TiME TICKETS ambayo ni wamiliki wa mfumo wa WEZESHAsasa wanatoa ushauri wa kiufundi kwa kutumia namba maalum isiyokuwa na malipo kwa muda wa masaa 24/7.

Uwazi na Uwajibikaji

 “ Mfumo wa WEZESHAsasa ni shirikishi  kwani unatoa fursa kwa mratibu wa zoezi la uchangiaji wa hiyari na kila mchangiaji mahala popote aliko kuweza kuona taarifa zote za msingi za harambee husika. Mchangiaji  anaweza kuipata huduma hii kupitia mtandao wa intaneti kwenye kompyuta au simu ya kiganjani. Uwazi mkubwa tuliouweka katika ubunifu huu unawafanya wachangiaji kuongeza imani kwa taasisi inayo ratibu harambee na hamasa ya kutaka kuendelea kuchangia zaidi ” Amesema Mkurugenzi wa Masoko TiME TICKETS, Mwasapi Kihongosi ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa WEZESHAsasa.

 

Kuhusu Kampuni ya TiME TICKETS

TiME TICKETS ni kampuni iliyoanzishwa nchini Tanzania na inasimamiwa na vijana wazawa wenye nia ya dhati kabisa ya kutoa majibu ya changamoto mbali mbali zenye kuzorotesha ukuwaji wa ustawi na maendeleo ya Watanzania hususani mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa fedha. TiME TICKETS ni  kampuni iliyobobea katika masuala TEHAMA na ni zao la miradi inayoratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia kupitia mradi wa Dar es Salaam Technohama Bussiness Incubator (DTBi). Ofisi kuu ya TiME Tickets ipo jengo la COSTECH, Kijitonyama barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Kwa maelezo zaidi tembelea www.timetickets.co.tz

 

 

Kufahamu maelezo zaidi ya mfumo wa WEZESHAsasa, tafadhali tembelea www.wezeshasasa.com. Kwa maulizo na msaada zaidi tuandikie kupitia taarifa@wezeshasasa.com au piga simu 0752030032

WEZESHAsasa Team, EcoValley Advisers team and Clouds media personel