WEZESHAsasa - Jukwa la Harambee

Je unahitaji kufanya harambee kwaajili ya mradi/ bidhaa au shughuli ya kimaendeleo? Tembelea sasa www.wezeshasasa.com kuanzisha harambee yako sasa! Je unahitaji msaada zaidi?
Wasiliana nasi kupitia taarifa@wezeshasasa.com au tupigie +255 752 030 032

 

WEZESHAsasa nini?

WEZESHAsasa ni jukwaa la mtandaoni lililoleta mapinduzi makubwa kwenye ukusanyaji wa michango kupitia harambee nchini Tanzania. Ni nyenzo ya kipekee na kisasa kabisa yenye kuwaunganisha moja kwa moja wachangishaji na wachangiaji wa harambee husika. Jukwaa hili linaweza kufikika kwa kutumia tovuti, vitumizi na hata kwa njia ya SMS (jumbe fupi) na hivyo kutoa nafasi zaidi ya kukua na kuwafikia watu wengi katika maeneo mbalimbali, ili mradi tu wawe na simu ya mkononi na huduma ya pesa za mtandao.

Kwa kutumia WEZESHAsasa, kila mtu alipo anaweza kuchangia na kufuatilia michango kulingana na lengo husika na kushuhudia michango ikiongezeka mubashara kadiri watu wanavyochangia. Kuona namba za simu za wachangiaji kwa ufupi, idadi na jumla ya michango moja kwa moja ni jambo la kipekee na muhimu sana kwani linaongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji na hivyo kuongeza imani na hamasa kwa wachangiaji.

Wachangishaji nao kwa upande mwingine huweza kupata taarifa nyingi zaidi za wachangiaji. Kwa kupitia WEZESHAsasa, wachangishaji huweza kupata na kupakua ripoti mbalimbali zenye kutoa taswira za maendeleo ya michango wakati wowote, mahali popote. Zaidi wanapata fursa ya kupata mawasiliano na kuunganishwa na watu wanaosapoti shughuli zao.

 

Kwanini WEZESHAsasa ni mfumo bora zaidi wa uchangishaji?

WEZESHAsasa ndio mfumo bora zaidi kutumia katika harambee kwasababu:

  1. Kutumia namba moja maalumu kukusanyia michango. Kwa kutumia namba moja maalumu inayofanana kwa mitandao yote ya simu, Mf. 180180, wachangiaji hupata urahisi zaidi wa kukumbuka taratibu za uchangiaji na kupunguza mkanganyiko.
     
  2. Kuwa na ukurasa maalumu wa harambe: Kila kampeni hupata ukurasa pekee katika tovuti ya www.wezeshasasa.com ambapo huweza kuweka maelezo na picha kuhusu harambee. Katika ukurasa huu, mchangishaji hupata nafasi ya kutoa maendeleo ya michango na mradi/ shughuli husika. Zaidi huweza kuweka taarifa za wadau wa harambee husika kuongeza kufahamika kwa wadau hao.
     
  3. Kushirikisha watu zaidi kupitia mitandao ya kijamii, SMS na barua pepe. Mfumo wa WEZESHAsasa pia una nyenzo maridadi zinazompa mtumiaji fursa ya kushirikisha marafiki na wadau mbalimbali habari za harambee husika. Hii huongeza mianya mingi ya kuwafikia watu na hivyo mafanikio zaidi ya harambee husika.
     
  4. Taarifa na maendeleo mubashara ya michango na wachangiaji. Upekee wa mfumo wa WEZESHAsasa ni kuwa michango yote na wachangiaji wanaongezeka moja kwa moja kila wanapochangia. Taarifa hii iko wazi kwa watu wote na huleta picha halisi ya ushiriki wa watu kwenye harambee husika. Mchangishaji huweza kupakua taarifa zote za wachangishaji na nyinginezo nyingi moja kwa moja kutoka kwenye tovuti ya www.wezeshasasa.com
     
  5. Huduma kwa wateja 24/7: Tuna wataalamu wetu ambao huhakikisha wanatoa msaada na maelekezo pale inabopidi ili kusaidi shughuli nzima za uchangishaji ziende vyema. Kutufikia timu WEZESHAsasa tafadhali tuandikie barua pepe kupitia taarifa@wezeshasasa.com au tupigie simu +255 752 030 032. Unaweza pia kutufuatilia na kuwasiliana nasi kupitia mitandao yetu ya kijamii: Twitter: @wezeshasasa, Facebook: @sasawezesha,  Instagram: @wezeshasasa