MRADI WA VIZIWI KAZI ZA MIKONO

MRADI WA VIZIWI KAZI ZA MIKONO

Reference No: 305030


I) TAARIFA YA TAASISI Viboko deaf ni kikundi kilianzishwa kwa viziwi watatu, kinafanya shughuli mbalimbali kupitia kazi ya mikono kwa kuuza bidhaa na kuzalisha bidhaa jipya. Kikundi kinalenga kuhakikisha kujiajiri kwa viziwi ambao kupata ujuzi wa ujasiriamali kama shughuli ya mikono kwa lengo la kupata mtaji endelevu. II) MAELEZO YA MRADI Tatizo ambalo mradi huu tunatarajia kulitatua ni kueneza upeo kwa jamii kuhusu viziwi kwamba wanaweza kufanya chochote kama wao bila ubaguzi na baada ya mradi kukua litaweza kupunguza hali ngumu ya viziwi na kuwahamasisha wazazi wenye viziwi kuleta kujiunga na kazi ya pamoja kikundi chetu Lengo la mradi linahusiana na tatizo tunalotaka kulitatua kwa kiasi cha Kuongeza mtaji wa kikundi na kueneza lugha ya alama kwa watu wa rika zote na kujenga udugu na urafiki kwa viziwi kuondokana na masuala ya kibaguzi. Kushirikiana na viziwi watatiwa moyo pindi kuanzisha mradi huu na ukawa na Mafanikio Mazuri itawavuta wengi kujiunga na Mradi huu. viziwi 10 wanakuja kikundi chetu na wanajifunza kufanya aina tofauti za viatu na batiki kutoka vifaa vyote vya viwanda na vya asili. Viziwi wako katika ngazi tofauti. Baadhi wameanza na wanajifunza jinsi ya kufanya kazi na vifaa. Baadhi ya wengine wanaanza kubuni bidhaa zao wenyewe. Kikundi chetu kinauza bidhaa na kuzalisha pesa kwa shughuli zote kupitia kazi ya mikono. MAONO YA MUDA MREFU: Kutuma viziwi 10 katika mpango wa mafunzo ya ufundi kila baada ya miezi 6. Kwa mpango wa kuzalisha mkondo wa kutosha wa walimu wapya na viziwi wanaotaka kujiunga na programu ya mafunzo ya ujuzi wa kazi za mikono III) MALENGO MAHUSUSI YA MRADI • Kubainisha, kuainisha na kutumia rasilimali za kazi za mikono. • Kuwawezesha viziwi kushiriki katika juhudi ya kuleta maendeleo. • Kusambaza masokoni bidhaa tunazotengeneza katika uzalishaji wa shughuli za mikono. • Kuwa na mipango mizuri ya ajira ambayo itawasaidia viziwi kutatua matatizo yao ya ukosefu wa ajira na kuwawezesha kujitegemea kiuchumi. • Kuwa na mtandao wa kupeana na kubadilishana habari kuhusu masoko. • Kuinua hali ya uchumi (kuondoa umasikini) kwa viziwi kujiwekea akiba. • Kusimamia na kujishughulisha na mradi huu kwa nia ya kupata pesa za kuwezesha kutekeleza malengo yao. • Kupata elimu ya ujasiriamali kwa viziwi.

Donated: 19,000 TZS
Goal: 5,000,000 TZS
0.38% Donated
Donation time is due
Supporters: 3

Recent Donations

255712****18
4,000 TZS

7 years ago Share


255752****32
10,000 TZS

7 years ago Share


255756****60
5,000 TZS

7 years ago Share


viboko deaf

Social:   
  0769940977
   vdegarusha@gmail.com


Viboko deaf ni kikundi kilianzishwa kwa viziwi watatu, kinafanya shughuli mbalimbali kupitia kazi ya mikono kwa kuuza bidhaa na kubuni bidhaa jipya

Leaderboard

1

10,000 TZS

255752****32 7 years ago
2

5,000 TZS

255756****60 7 years ago
3

4,000 TZS

255712****18 7 years ago