MAMA YETU YU HAI
Reference No: 430043
MAELEZO MAFUPI YA MRADI/KAMPENI Katika harakati za kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa maeneo ya vijijini, hospitali ya Rulenge imeonelea ni vema ishirikishe wadau na watu wote wenye mapenzi mema, katika kuharakisha mkakati wa ujenzi wa jengo jipya la huduma ya upasuaji kwa wakina mama wajawazito na watoto wachanga. Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma yenye kukidhi haja kufuatia kutokuwepo kwa jengo lenye sifa. Kutokuwepo kwa jengo lenye kukidhi vigezo na vifaa tiba husika, wakati mwingine kumepelekea kutokea kwa vifo vya wakina mama na watoto hata baada ya upasuaji. Ubora wa huduma ya wakina mama na watoto ni moja ya malengo yaliyomo ndani ya mpango mkakati wa hospitali wa 2017 -2022. LENGO MAHUSUSI LA HARAMBEE Harambee hii inatarajiwa kuwezesha kumalizia ujenzi wa nyumba ya kina mama wajawazito, upanuzi wa jengo la upasuaji na kuwezesha manunuzi ya vifaa tiba.
Goal: 43,834,532 TZS
Recent Donations

100 TZS
7 years ago Share

2,000 TZS
7 years ago Share

200 TZS
7 years ago Share

100 TZS
7 years ago Share

1,000 TZS
7 years ago Share

500 TZS
7 years ago Share

500 TZS
7 years ago Share

1,000 TZS
7 years ago Share

500 TZS
7 years ago Share

50,000 TZS
7 years ago Share
Rulenge Hospital
Social:255768730680
fredrickmry@yahoo.com
Hospitali ya Rulenge ni moja ya miundo mbinu inayopatikana katika wilaya ya Ngara ikiwa na dhamira ya kutoa huduma bora ya afya. Hospitali hii ilianzishwa kama zahanati kwa ufadhili wa watawa wenye asili ya nchi ya Canada mwaka 1952. Hospitali inazungukwa na wakazi wapatao 117,313 na ikiwa imeendelea kutoa huduma za afya kwa wananchi wasiopungua 8,680 kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012. Eneo la inamopatikana hospitali ya Rulenge ni tarafa ya Bushubi, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera. Hospitali iko umbali wa km 45 kutoka makao makuu ya wilaya ya Ngara na umbali wa km 350 kutoka makao makuu ya Mkoa. Hospitali hii inatoa huduma ya wagonjwa wa kulazwa na wale wa nje ili hali ikiwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 80 kwa wakati mmoja. Vile vile hospitali ya Rulenge hutumika kama hospitali ya rufaa kwa vituo viwili vya afya na zahanati 21 zilizomo ndani ya wilaya ya Ngara.