UJENZI WA SHULE MAALUMU YA WAATHIRIKA WA MIMBA ZA UTOTONI
Reference No: 210210
Habari. Naitwa Carol Ndosi, ni Mtanzania mpenda maendeleo na haswa kumuinua mtoto wa kike, mwanamke na Kijana kwenye jamii. Julai 2017, mtoto wa kike aliyepata ujauzito alisisitiziwa marfuku kurudi shule ya serikali baada ya kujifungua na kuendelea na masomo yake. Tunapoendelea na juhudi za kuhakikisha haki ya mtoto wa kike inalindwa, haswa haki ya elimu na kumaliza shule; hatuwezi kuwaacha wale waliothirika nyuma. Mimba nyingi PIA za utotoni zinatokana na vitendo vya ubakaji na ndoa za utotoni. Wengi wa hawa waathirika wanatoka kwenye mazingira magumu sana. Kukatishwa kwa masomo kunazidi kuturudisha nyumba kama jamii na taifa kimaendeleo. Tunahitaji nguvu kazi ya kuendele kulijenga taifa hili. Hawa walioathirika na mimba za utotoni ni nguvu kazi ya taifa. Tumeamua kuwajengea shule Mamaendeleo Vocational Residential Academy ambayo itatoa mafunzo ya elimu yatakayomwezesha huyu mtoto wa kike kuendelea na ndoto zake na maarifa ya kuweza kuajiriwa au kujiajiri kwenye fani mbali mbali. Sisi tuna kiwanja na nguvu kazi ya kuhakikisha tunafikia lengo hili. HATUWEZI wenyewe. Hili ni letu WOTE. Kumbuka zaidi ya 21% ya watoto wa kike kati ya miaka 15-19 hawamalizi shule kutokana na mimba kwa mujibu wa takwimu za NBS. We need to do this for the girl child. The girl child who has been abused, abandoned forgotten and now banned.
Goal: 100,000,000 TZS
Recent Donations

5,000 TZS
6 years ago Share

2,500 TZS
7 years ago Share

10,000 TZS
7 years ago Share

10,000 TZS
7 years ago Share

10,000 TZS
7 years ago Share

2,500 TZS
7 years ago Share

25,000 TZS
7 years ago Share

7,000 TZS
7 years ago Share

50,000 TZS
7 years ago Share

5,000 TZS
7 years ago Share
Tunapoendelea na juhudi za kuhakikisha haki ya mtoto wa kike inalindwa, haswa haki ya elimu na kumaliza shule; hatuwezi kuwaacha wale waliothirika nyuma. Mimba nyingi PIA za utotoni zinatokana na vitendo vya ubakaji na ndoa za utotoni. Wengi wa hawa waathirika wanatoka kwenye mazingira magumu sana. Kukatishwa kwa masomo kunazidi kuturudisha nyumba kama jamii na taifa kimaendeleo. Tunahitaji nguvu kazi ya kuendele kulijenga taifa hili. Hawa walioathirika na mimba za utotoni ni nguvu kazi ya taifa. Tumeamua kuwajengea shule Mamaendeleo Vocational Residential Academy, itatoa mafunzo ya elimu yatakayomwezesha huyu mtoto wa kike kuendelea na ndoto zake na maarifa ya kuweza kuajiriwa au kujiajiri kwenye fani mbali mbali. Sisi tuna kiwanja na nguvu kazi ya kuhakikisha tunafikia lengo hili.HATUWEZI wenyewe. Hili ni letu WOTE. Kumbuka zaidi ya 21% ya watoto wa kike kati ya miaka 15-19 hawamalizi shule kutokana na mimba kwa mujibu wa takwimu za NBS. We need to do this for the girl child. The girl child who has been abused, abandoned forgotten and now banned.