
Afya Kwanza.
Reference No: 100200013
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tai Tanzania inayojishughulisha na utoaji wa elimu juu ya masuala mbalimbali kupitia katuni za chapa tatu, inalenga kufadhili wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu hususani wasichana, katika shule ya Sekondari Mongola, iliyopo Morogoro. Ufadhili huo utajumuisha ugawaji wa barakoa kwa ajili ya kujikinga na Uviko-19, taulo za kike (pedi), na sabuni.
Mnamo mwaka jana tulifanikiwa kufadhili wanafunzi 16 wa kidato cha 4 mahitaji yao ya shule tukishirikiana na Kipaji Foundation, na wote walifanikiwa kufaulu vizuri. Na mwaka huu tunalenga kufikisha kiasi cha shilingi million mbili(2,000,000) ili kuweza kugawa vifaa hivyo kwa wanafunzi wenye uhitaji na kuwapa elimu juu ya masuala ya afya.
Goal: 2,000,000 TZS
Recent Donations

15,000 TZS
3 years ago Share

20,000 TZS
3 years ago Share

2,000 TZS
3 years ago Share

1,000 TZS
3 years ago Share
Tai Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali linalotumia teknolojia ya media kutoa taarifa juu ya maswala ya afya, elimu na haki za kijamii. Tai Tanzania inazingatia kutoa elimu bora kwa jamii, Tunatumia katuni chapa tatu (3D animations) kufikisha ujumbe kwa hadhira husika, ambao ni wasichana na wavulana waliopo katika rika balehe.