MSAIDIE RUSSELL AWEZE KUTEMBEA

MSAIDIE RUSSELL AWEZE KUTEMBEA

Reference No: 692703


Mwanangu Russell alizaliwa tarehe 23 Dec 2008, na alizaliwa mzima wa afya. Mnamo mwaka 2010 akiwa na mwaka na miezi 3 alipata degedege na wiki mbili baadae Pneomonia (Nimonia) kali na kulazwa ICU kwa muda wa mwezi mmoja. Akiwa ICU aliingia kwenye Coma kwa mda wa siku 10 Alipozunduka madaktari wakaona hajarudi kwenye hali yake ya kawada. Akafanyiwa vipimo vya ziada na ikagundulika baadhi ya seli za ubongo ziliharibika na sasa ni mtoto mwenye Mtindio wa ubongo (Cerebral Palsy) pia kupata ukipofu wa muda (short term blindness). Pia Pneomonia ilisababbisha mapafu na moyo wake kujaa maji na kufanya kazi asilimia 18 tu, lakini kwa kutumia dawa ndani ya mwaka tulifanikiwa kutibu Moyo. Maradhi haya yakamfanya kuwa mtoto tegemezi asiyeweza kukaa,kuongea, wala kutembea hadi hii leo. Tunamkazania na mazoezi ya viungo kila siku. Mwaka huu 2018 nilitambulishwa kwa hospitali iitwayo NeuroGen Brain and Spine Institute @NeuroGenBSI iliyoko Mumbai, India hospitali hii ni mabigwa wa kutoa matibabu kupitia Stem Cell Therapy. Stem cell transplantation ni matibabu ambayo hizo seli (stem cells) huchukuliwa kwenyebuti wa mgongo wa mtoto (bone marrow) hutenganishwa na mtoto anachomwa hizo seli zake kwenye uti wa mgogo na zinasafirishwa kwenda kwenye ubongo moja kwa moja na kwenda kuziba nafasi ya seli zilizoharibika. Kupitia tiba hii Russell atapata nafasi ya kupambana na maradhi yake na akijaliwa ataweka kujitegemea mwenyewe (akakaa, akaongea, na kutembea) kwani imeonyesha mafanikio makubwa ya asilimia 60 kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 12, ambapo wengine wamepona kabisa. Anahitaji kuelekea India mnamo Januari 24, 2019 kwa matibabu hayo na tutakaa huko kwa mda wa wiki 2. Gharama za matibabu na safari kiujumla ni USD13,000 ambayo ni Takribani Tsh 30million. Kama mzazi (Single Parent) sina uwezo wa kukimu gharama za safari ya matibabu, narejea kwenu kuomba msaada wa michango ya kifedha ili nifanikishe malengo na kumpa mwanangu nafasi ya kukua kama watoto wengine. Natanguliza shukrani za dhati, Mungu awabariki. ZIMEBAKI SIKU CHACHE SANA.. Mchango wowote utasaidia.. Changia chochote ulichonacho ni kikubwa sana kwetu..

Donated: 0 TZS
Goal: 30,000,000 TZS
0.00% Donated
Donation time is due
Supporters: 0

Recent Donations

Tayanah Tibenda

Social:   
  0717746979
   tayanahtibenda@gmail.com


Mama Mzazi wa Rusell, Single Parent living in Arusha, Tanzania.

Leaderboard