MSAIDIE RUSSELL AWEZE KUTEMBEA

MSAIDIE RUSSELL AWEZE KUTEMBEA

Mwanangu Russell alizaliwa tarehe 23 Dec 2008, na alizaliwa mzima wa afya. Mnamo mwaka 2010 akiwa na mwaka na miezi 3 alipata degedege na wiki mbili baadae Pneomonia (Nimonia) kali na kulazwa ICU kwa muda wa mwezi mmoja. Akiwa ICU aliingia kwenye Coma kwa mda wa siku 10 Alipozunduka madaktari wakaona hajarudi kwenye hali yake ya kawada. Akafanyiwa vipimo vya ziada na ikagundulika baadhi ya seli za ubongo ziliharibika na sasa ni mtoto mwenye Mtindio wa ubongo (Cerebral Palsy) pia kupata ukipofu wa muda (short term blindness). Pia Pneomonia ilisababbisha mapafu na moyo wake kujaa maji na kufanya kazi asilimia 18 tu, lakini kwa kutumia dawa ndani ya mwaka tulifanikiwa kutibu Moyo. Maradhi haya yakamfanya kuwa mtoto tegemezi asiyeweza kukaa,kuongea, wala kutembea hadi hii leo. Tunamkazania na mazoezi ya viungo kila siku. Mwaka huu 2018 nilitambulishwa kwa hospitali iitwayo NeuroGen Brain and Spine Institute @NeuroGenBSI iliyoko Mumbai, India hospitali hii ni mabigwa wa kutoa matibabu kupitia Stem Cell Therapy. Stem cell transplantation ni matibabu ambayo hizo seli (stem cells) huchukuliwa kwenyebuti wa mgongo wa mtoto (bone marrow) hutenganishwa na mtoto anachomwa hizo seli zake kwenye uti wa mgogo na zinasafirishwa kwenda kwenye ubongo moja kwa moja na kwenda kuziba nafasi ya seli zilizoharibika. Kupitia tiba hii Russell atapata nafasi ya kupambana na maradhi yake na akijaliwa ataweka kujitegemea mwenyewe (akakaa, akaongea, na kutembea) kwani imeonyesha mafanikio makubwa ya asilimia 60 kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 12, ambapo wengine wamepona kabisa. Anahitaji kuelekea India mnamo Januari 24, 2019 kwa matibabu hayo na tutakaa huko kwa mda wa wiki 2. Gharama za matibabu na safari kiujumla ni USD13,000 ambayo ni Takribani Tsh 30million. Kama mzazi (Single Parent) sina uwezo wa kukimu gharama za safari ya matibabu, narejea kwenu kuomba msaada wa michango ya kifedha ili nifanikishe malengo na kumpa mwanangu nafasi ya kukua kama watoto wengine. Natanguliza shukrani za dhati, Mungu awabariki. ZIMEBAKI SIKU CHACHE SANA.. Mchango wowote utasaidia.. Changia chochote ulichonacho ni kikubwa sana kwetu..

Zimechangwa: 0 TZS 0.00%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 692703

Msaada kwa Fruitful Orphanage and Daycare centre

Msaada kwa Fruitful Orphanage and Daycare centre

Hi Friends! Nimeanzisha hii campaign kwa ajili ya kusaidia watoto yatima waliopoko kwenye kituo cha Fruitful Orphanage and Daycare Centre. Kiasi chote kitapelekwa kwenye kituo ilikusaidia watoto upande wa chakula. Nitashukuru kwa mchango wowote utakaochangwa.

Zimechangwa: 0 TZS 0.00%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 176542

RUDISHA TABASAMU LA ARNOLD

RUDISHA TABASAMU LA ARNOLD

Naitwa Arnold Augustine, nina miaka 25, ni yatima, ni mwanafunzi wa udaktari mwaka wa 5 katika chuo cha tiba KCMC Moshi. Niligundulika kuwa na ugonjwa wa figo kushindwa kufanya kazi (Chronic Renal Failure) na nimekuwa nikifanyiwa uchujaji wa damu kwa kutumia mashine maalum (Hemodialysis). Matibabu ya moja kwa moja ya ugonjwa huu ni kupandikizwa figo. Niwashukuru sana wanafunzi wenzangu, uongozi wa chuo na hospitali kwa msaada wao mpaka nilipofikia. Nawaomba sana watanzania mnisaidie kunichangia ili niweze kufanyiwa upandishaji huo. ASANTENI SANA NA MUNGU AWABIRIKI. NB: Michango hii ya mtandaoni inaratibiwa na Gideon Barongo (0765023986) kwa ruhusa yangu Arnold Augustine (0766693883)

Zimechangwa: 1,152,300 TZS 3.84%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 303030

Send high school entrepreneurs to a pitch competition in United States

Send high school entrepreneurs to a pitch competition in United States

We are a group of high school students in Tanzania from Outpeak a project that helps needy yet smart Girls in secondary school. In Tanzania there are 1.5 million adolescents not in school right now due to different obstacles like inadequate scholastic materials, lack of sanitary pads and bus fare, which hinders girls from going to school thus increasing the risk of poverty and gender based violence in her future . Our Solution: we decided to empower smart yet poor girls who are in secondary level by creating a frundrasing platform ( www.outpeak.org ) to help them raise funds to support their basic needs. We incubate their small business project by providing seed income and mentorship so that they could financially uproot their families and themselves and not depend on donations. Our Impact: -So far we have supported 6 girls with scholastic materials for one year and we want to recruit second batch -We have run two successful crowdfunding events and partnered with 2 different school to post our donation box and help their girls. -We have won two seed income competitions and we are still implementing the project. Our Why: We decided to invest in girl education because a graduate is less likely to get HIV, have children that die under the age of 5 and will raise her community’s economy tremendously, and also it is the most undermined group that has a lot of potential and a promising future of the nation Our Need: We are humbly asking you to support us to raise money for airtfare and visa fees to travel to the Final competition in USA. This year we had the opportunity to pitch in the Diamond challenge regional competition organised by the University of Dar es salaam, Tanzania and won the 1st Prize, As regional winners we are to compete in the final global competition which will be held at Delaware in USA from 11th April to 13th April to pitch and compete for $10,000 seed income. http://www.shakila.co.tz/2018/03/05/diamond-challenge-in-tanzania/ http://diamondchallenge.org/ We need 7000$ which includes: - $650 for each one’s visa - $6350 for round-trip travel cost from Tanzania to Delaware - USA Support us and give a Tanzania girl a chance to good education. Kindly share with your network. Asante Sana !! ========================================= ============ kwa kiswahili ============================= Sisi ni kikundi cha wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania kutoka kwa mradi wa Outpeak ambao husaidia wasichana wanaohitaji lakini hufaulu kwa hali ya juu waliopo katika shule ya sekondari. Tanzania kuna vijana milioni 1.5 wasio shuleni kwa sasa kutokana na vikwazo tofauti kama vifaa vya kutosha vya kusomea, ukosefu wa pads safi na n.k, ambavyo huzuia wasichana kwenda shule na hivyo kuongeza hatari ya umaskini na unyanyasaji wa kijinsia katika siku zijazo. Suluhisho Letu: tuliamua kuwawezesha wasichana wenye ufaulu lakini maskini ambao ni katika ngazi ya sekondari kwa kuunda jukwaa la ufadhili (www.outpeak.org) kuwasaidia kuongeza fedha ili kusaidia mahitaji yao ya msingi. Tunashirikisha mradi wao wa biashara ndogo ndogo kwa kutoa mapato na ushauri wa ujasiriamali ili waweze kufadhili familia zao na wao wenyewe na sio kutegemea mchango. Impact yetu: Kwa hivyo tumeunga mkono wasichana 6 wenye vifaa vya elimu kwa mwaka mmoja na tunataka kuunda kundi la pili - Tumeendesha matukio mawili ya fedha ya umati wa watu na kushirikiana na shule 2 tofauti ili kuwasilisha sanduku la mchango wetu na kuwasaidia wasichana wao. - Tulishinda mtaji wa millioni moja na laki 3 kupata ushindani huo tunatekeleza mradi huu. Kwa nini: Tuliamua kuwekeza katika elimu ya shule kwa sababu mhitimu hawezi kupata VVU, kuwa na watoto ambao hufa chini ya umri wa miaka 5 na watainua uchumi wa jamii yake kwa kiasi kikubwa, na baadaye wa taifa Uhitaji wetu: Tunakuomba kwa unyenyekevu kutusaidia ili kuongeza fedha kwa ajili ya tiketi za ndege na kusafiri kwenye mashindano mwisho nchini Marekani. Mwaka huu tulishinda fursa ya kushiriki katika ushindani wa kikanda wa Diamond Challenge ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Tanzania na kushinda tuzo ya kwanza, kama washindi wa kikanda tunapaswa kushindana katika ushindani wa mwisho wa kimataifa ambao utafanyika Delaware. MAREKANI. kuanzia 11 Aprili hadi 13 Aprili kwenda na kushindana kwa kipato cha dola 10,000. http://diamondchallenge.org/ http://www.shakila.co.tz/2018/03/05/diamond-challenge-in-tanzania/ Tunahitaji dola 7000 ambazo zinajumuisha: - $ 650 kwa kila visa - $ 6350 kwa gharama za usafiri wa safari ya kurudi kutoka Tanzania hadi Delaware - USA Tusaidie kumpa msichana waki Tanzania fursa ya elimu nzuri. Fanya kushiriki kwa mtandao wako. Asante sana !!

Zimechangwa: 0 TZS 0.00%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 550055

Mchango wa Operesheni ya Figo - Mwl. Kisese

Mchango wa Operesheni ya Figo - Mwl. Kisese

Mimi naitwa mwalimu Kisese ( Charles Kisese), naumwa sana na ninaomba msaada wa kifedha. Figo zote mbili hazifanyi kazi, moyo umetanuka na maini yamevimba. Madaktari bingwa wa figo na moyo wa Muhimbili walipokaa meza moja pamoja nami mwezi huu wa pili 2018, wamesema madhara yote hayo chanzo ni figo kutofanya kazi, wakashauri nifanyiwe upandikizaji wa figo ( Kidney transplant) kwanza. Gharama za upasuaji pamoja na Figo ni Milioni 25, (25,000,000/-). Natarajiwa kufanyiwa operesheni mwezi wa nne katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Gharama hiyo ni kubwa na nashindwa kuibeba maana nimeumwa Kwa muda mrefu, tangu 2015. Kwa ujumbe huu nakuomba ndugu yangu unichangie kiasi chochote utakachojaliwa ili kupata fedha hizo Kwa wakati. Nisaidie pia kuwafikishia watu wengine taarifa hizi. Mungu akubariki sana. Kwa sasa hivi ninaishi Kimara, Dar es Salaam. Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana: Mwl. Kisese 0755811967 au 0711629415. Pia unaweza kuwasiliana na Mke Wangu 0756542303

Zimechangwa: 2,489,400 TZS 9.96%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 252525

Rambirambi kwa familia ya Akwilina Akwilin

Rambirambi kwa familia ya Akwilina Akwilin

Akwilina Akwilini alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Akwilina alifariki tarehe 16/02/2017 kwa kupigwa risasi wakati ambao askari wa Jeshi la Polisi walirusha risasi kutawanya waandamanaji waliohusishwa na shughuli za kampeni za Uchaguzi Mdogo wa marudio wa Ubunge katika jimbo la Kinondoni. Akwilina, akitokea katika familia ya mtanzania wa kawaida kabisa, alikuwa ni tumaini la familia. Kama Watanzania wenzake, tunaamini ni muhimu kusaidia kufuta machozi kwa ndugu, na familia ya Akwilini kwa kuwawezesha kwa kile kidogo tulichojaaliwa nacho, ingawa utoaji huu hautoondoa ukweli kwamba hatuwezi kumrudisha aliyetutoka, lakini utaleta maana ya upendo, mshikamano na umoja wa Kitanzania wakati wa matatizo kama ilivyo wakati wa furaha. Hivyo basi, tunakuomba uungane na wazazi na familia ya Akwilina kwa kuchangia kidogo ulichojaaliwa kuwezesha mipango ya mazishi na maombolezo ya mpendwa wao, ambaye pia ni mpendwa wetu kwakuwa Akwilina alitokea familia ya chini, na familia ilikua inamtegemea aje kuwakomboa pindi amalizapo masomo yake ya Chuo. Mchango huu unaratibiwa na, Bi Segolena Richard Wisso (+255765171191), ambaye ni Mama Mlezi wa Marehemu Akwilina Akwilini Upumzike kwa Amani, Akwilina Akwilin

Zimechangwa: 436,500 TZS 8.73%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 160160

UJENZI WA SHULE MAALUMU YA WAATHIRIKA WA MIMBA ZA UTOTONI

UJENZI WA SHULE MAALUMU YA WAATHIRIKA WA MIMBA ZA UTOTONI

Habari. Naitwa Carol Ndosi, ni Mtanzania mpenda maendeleo na haswa kumuinua mtoto wa kike, mwanamke na Kijana kwenye jamii. Julai 2017, mtoto wa kike aliyepata ujauzito alisisitiziwa marfuku kurudi shule ya serikali baada ya kujifungua na kuendelea na masomo yake. Tunapoendelea na juhudi za kuhakikisha haki ya mtoto wa kike inalindwa, haswa haki ya elimu na kumaliza shule; hatuwezi kuwaacha wale waliothirika nyuma. Mimba nyingi PIA za utotoni zinatokana na vitendo vya ubakaji na ndoa za utotoni. Wengi wa hawa waathirika wanatoka kwenye mazingira magumu sana. Kukatishwa kwa masomo kunazidi kuturudisha nyumba kama jamii na taifa kimaendeleo. Tunahitaji nguvu kazi ya kuendele kulijenga taifa hili. Hawa walioathirika na mimba za utotoni ni nguvu kazi ya taifa. Tumeamua kuwajengea shule Mamaendeleo Vocational Residential Academy ambayo itatoa mafunzo ya elimu yatakayomwezesha huyu mtoto wa kike kuendelea na ndoto zake na maarifa ya kuweza kuajiriwa au kujiajiri kwenye fani mbali mbali. Sisi tuna kiwanja na nguvu kazi ya kuhakikisha tunafikia lengo hili. HATUWEZI wenyewe. Hili ni letu WOTE. Kumbuka zaidi ya 21% ya watoto wa kike kati ya miaka 15-19 hawamalizi shule kutokana na mimba kwa mujibu wa takwimu za NBS. We need to do this for the girl child. The girl child who has been abused, abandoned forgotten and now banned.

Zimechangwa: 136,500 TZS 0.14%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 210210

Be The Light for IJANGO ZAIDIA Orphanage at Sinza Madukani

Be The Light for IJANGO ZAIDIA Orphanage at Sinza Madukani

TAI Tanzania is an organization focusing on improving health, hygiene, and education in the community. This campaign aims at raising funds to support 84 children living at the center through providing them with hygiene products, health insurance and school uniform. Your donation will make an immediate difference in the lives of the children at Ijango Zaidia Orphanage Center. "WE MAKE A LIVING BY WHAT WE MAKE A LIFE BY WHAT WE GIVE" - Winston Churchill

Zimechangwa: 128,000 TZS 2.90%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 440044

Stretch Scoliosis and Stand Tall with Zainab

Stretch Scoliosis and Stand Tall with Zainab

Zainab is among the sweetest soul you can meet. A 17-year-old pretty girl who just completed form four. She is tough she has dreams but it's her back pains that gives some hindrance. Let us spread some love and touch this beautiful soul life by joining hands to support her surgery that is to be held in Ghana early next year. Let us stretch the severe scoliosis and stand tall with Zainab. Standtallinternational is the institution responsible for this campaign. The main coordinators are Masha Balovenkov (+1 (443) 739-9462), Martin Ngonyani (+255 787 682 032) and Esther Matemba (0752288569) As one person I can not change the world by I can change the world of one small person.

Zimechangwa: 3,525,000 TZS 35.25%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 150180

MRADI WA VIZIWI KAZI ZA MIKONO

MRADI WA VIZIWI KAZI ZA MIKONO

I) TAARIFA YA TAASISI Viboko deaf ni kikundi kilianzishwa kwa viziwi watatu, kinafanya shughuli mbalimbali kupitia kazi ya mikono kwa kuuza bidhaa na kuzalisha bidhaa jipya. Kikundi kinalenga kuhakikisha kujiajiri kwa viziwi ambao kupata ujuzi wa ujasiriamali kama shughuli ya mikono kwa lengo la kupata mtaji endelevu. II) MAELEZO YA MRADI Tatizo ambalo mradi huu tunatarajia kulitatua ni kueneza upeo kwa jamii kuhusu viziwi kwamba wanaweza kufanya chochote kama wao bila ubaguzi na baada ya mradi kukua litaweza kupunguza hali ngumu ya viziwi na kuwahamasisha wazazi wenye viziwi kuleta kujiunga na kazi ya pamoja kikundi chetu Lengo la mradi linahusiana na tatizo tunalotaka kulitatua kwa kiasi cha Kuongeza mtaji wa kikundi na kueneza lugha ya alama kwa watu wa rika zote na kujenga udugu na urafiki kwa viziwi kuondokana na masuala ya kibaguzi. Kushirikiana na viziwi watatiwa moyo pindi kuanzisha mradi huu na ukawa na Mafanikio Mazuri itawavuta wengi kujiunga na Mradi huu. viziwi 10 wanakuja kikundi chetu na wanajifunza kufanya aina tofauti za viatu na batiki kutoka vifaa vyote vya viwanda na vya asili. Viziwi wako katika ngazi tofauti. Baadhi wameanza na wanajifunza jinsi ya kufanya kazi na vifaa. Baadhi ya wengine wanaanza kubuni bidhaa zao wenyewe. Kikundi chetu kinauza bidhaa na kuzalisha pesa kwa shughuli zote kupitia kazi ya mikono. MAONO YA MUDA MREFU: Kutuma viziwi 10 katika mpango wa mafunzo ya ufundi kila baada ya miezi 6. Kwa mpango wa kuzalisha mkondo wa kutosha wa walimu wapya na viziwi wanaotaka kujiunga na programu ya mafunzo ya ujuzi wa kazi za mikono III) MALENGO MAHUSUSI YA MRADI • Kubainisha, kuainisha na kutumia rasilimali za kazi za mikono. • Kuwawezesha viziwi kushiriki katika juhudi ya kuleta maendeleo. • Kusambaza masokoni bidhaa tunazotengeneza katika uzalishaji wa shughuli za mikono. • Kuwa na mipango mizuri ya ajira ambayo itawasaidia viziwi kutatua matatizo yao ya ukosefu wa ajira na kuwawezesha kujitegemea kiuchumi. • Kuwa na mtandao wa kupeana na kubadilishana habari kuhusu masoko. • Kuinua hali ya uchumi (kuondoa umasikini) kwa viziwi kujiwekea akiba. • Kusimamia na kujishughulisha na mradi huu kwa nia ya kupata pesa za kuwezesha kutekeleza malengo yao. • Kupata elimu ya ujasiriamali kwa viziwi.

Zimechangwa: 19,000 TZS 0.38%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 305030

Rudisha Furaha kwa Judith

Rudisha Furaha kwa Judith

Judith Mushi ni binti mwenye miaka 20. Alizaliwa akina na changamoto ya ulemavu wa macho, kuongea, akili na tatizo la koo. kwasasa anaishi na mama yake tu Bi Hilda Mushi baada ya baba yake kufariki kwa ugonjwa wa kisukari. Judith alifanyiwa operesheni mara 6 hospitali ya Muhimbili na kuhamishiwa CCRBT. Anahitaji msaada wa chochote kubadili maisha yake. Mchango huu umelenga kumsaidia Judith kupata bima ya afya, matibabu na kuiwezesha familia yake ili iweze kumhudumia kwa urahisi. Michango hii itasaidia pia kuiwezesha familia ya Judith kiuchumi na kuwatoa katika hali ya kuwa tegemezi waweze kuendelea kujitegemea katika kumhudumia Judith Michango hii inaratibiwa na PLPDF, mawasiliano zaidi piga simu +255 713 889 861

Zimechangwa: 269,414 TZS 5.39%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 161616

JIPU NDANI YA UBONGO

JIPU NDANI YA UBONGO

Kuchapisha kitabu cha Simulizi la kweli, JIPU NDANI YA UBONGO, Kueleza kwa kirefu juu ya uzoefu wangu wa uvimbe mkubwa niliokuwa nao kwenye ubongo, jinsi ulivyoniathiri, matibabu yake na uponyaji wake, lengo likiwa kuelimisha jamii kuhusiana na afya zao hasa kwa magonjwa makubwa na ya hatari, na kuwatia moyo wale waliopata matatizo yenye kukatisha tamaa kuwa yupo Mungu awezaye kufanya yaliyoshindikana kwa wanadamu

Zimechangwa: 14,200 TZS 0.24%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 101010

MAMA YETU YU HAI

MAMA YETU YU HAI

MAELEZO MAFUPI YA MRADI/KAMPENI Katika harakati za kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa maeneo ya vijijini, hospitali ya Rulenge imeonelea ni vema ishirikishe wadau na watu wote wenye mapenzi mema, katika kuharakisha mkakati wa ujenzi wa jengo jipya la huduma ya upasuaji kwa wakina mama wajawazito na watoto wachanga. Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma yenye kukidhi haja kufuatia kutokuwepo kwa jengo lenye sifa. Kutokuwepo kwa jengo lenye kukidhi vigezo na vifaa tiba husika, wakati mwingine kumepelekea kutokea kwa vifo vya wakina mama na watoto hata baada ya upasuaji. Ubora wa huduma ya wakina mama na watoto ni moja ya malengo yaliyomo ndani ya mpango mkakati wa hospitali wa 2017 -2022. LENGO MAHUSUSI LA HARAMBEE Harambee hii inatarajiwa kuwezesha kumalizia ujenzi wa nyumba ya kina mama wajawazito, upanuzi wa jengo la upasuaji na kuwezesha manunuzi ya vifaa tiba.

Zimechangwa: 196,400 TZS 0.45%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 430043

Jali Campaign - Support Girls Education

Jali Campaign - Support Girls Education

Girls in public schools of Tanzania skips schools because they face problems of purchasing the sanitary pads. Financial stability limits them and hence they just move out of schools without any further education. At TAI Tanzania, we are an NGO where one of the projects is to provide sanitary pads to 12 girls in government schools for an entire year. We manage to get donations from visitors in supermarkets who buy sanitary pads and drop in the Binti Box around the counter. Binti Box means a girl Box in the local Swahili language. GOAL: This year 2017, we have a target to reach 5000 pads for 1500 girls. Until now, we have managed to raise 400 pads. We are looking forward to address this issue online too. Target: 10 public schools, and 120 girls to receive pads for an entire year. Furthermore, educating these youth in the month of July to August in the subjects of Reproductive Health and Menstrual Hygiene by volunteers and interns both local and international is also done. We get these young minds to be critical thinkers and empower them where class facilitators create awareness and teach them about all these issues faced. Below is a link of how Jali Project is carried out during the summer https://www.youtube.com/watch?v=6656AsbteGY Your contributions to this project will highly be appreciated and be catered in the project delivery during the summer time in the regions of Morogoro and Dar es Salaam. Kindly donate to enable these girls to remain in schools and to manage their menses as well. A small pack of sanitary pad can support a girl for a whole month. For more information, please follow this link https://www.tai.or.tz/ Thank you for showing your support, TAI Team

Zimechangwa: 201,700 TZS 2.88%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 694044

Stand Tall With Jay

Stand Tall With Jay

Let's join hands and be part of the amazing life changing journey for our little pretty angel Jamila. She is a 12 year old child suffering from severe progressive scoliosis. We are raising $5000 (about TZS 10,000,000) to support her spine surgery that will be done in Texas USA during the month August 2017. Standtall International is the the institution responsible for this campaign. The main coordinators are Masha Balovenkov (+14437399462), Esther Matemba (0752288569) and Martin Ngonyani (0787682032) "AS ONE PERSON I CAN NOT CHANGE THE WORLD BUT I CAN CHANGE THE WORLD OF ONE SMALL PERSON..."

Zimechangwa: 781,100 TZS 7.81%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 808080

Rudisha Tabasamu - 100 MOYO

Rudisha Tabasamu - 100 MOYO

Kuwa sehemu ya harambee hii muhimu ya kuchangisha milioni 200 kwaajili ya matibabu ya watoto 100 ambao wana matatizo ya moyo. Gharama ya kila mtoto ni milioni 2. Watoto hawa watafanyiwa watatibiwa katika hospitali ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) iliyoko Muhimbili. Kampeni hii inasimamiwa na taasisi ya Jakaya Kikwete Cardiac Insitute (JKCI) na kuraibiwa na Clouds Media Kwa mawasiliano zaidi piga +255 652 860 991

Zimechangwa: 2,828,800 TZS 1.41%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 100100

HELP LOYOLA STUDENTS TO DEVELOP DRONES FOR DELIVERING MEDICINES IN RURAL AREAS  IN TANZANIA

HELP LOYOLA STUDENTS TO DEVELOP DRONES FOR DELIVERING MEDICINES IN RURAL AREAS IN TANZANIA

Outside the capital, Dar Es Salaam, medical services can be patchy. Remote areas often lack hospitals and medical centers can be long distances away for rural communities. Project Idea: Designing and making Drones for delivering medicines in the rural area. We are going design and make drones and write the web and mobile applications to make it run. This school students together with the teacher came up with an idea of making drones can deliver medicines in the rural areas. As we have seen in many occasions these students are good at making hardware and software and they have got award locally, nationally and internationally we try to make a drone test to deliver medicines. PROBLEM STATEMENT These students need hardware that is parts of drones to assemble and make software to make it run. We came to realize that the parts of the drones are so expensive and we can get only in America. Also, we need heavy batteries and motors to make it run. The project will be monitored by both the project manager and the head of school. The project manager will be in charge of evaluation of the programme which will be done after six months that is, December and June. However, there are some expenses associated with the project which includes; -Transport for importing the drone parts -Place to work with High Speed internet -Transport, food and work allowance for the students until the drone is made real. After that, the students become full-time employees for making drones and implementing.

Zimechangwa: 0 TZS 0.00%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 153015

Narudisha Tabasamu

Narudisha Tabasamu

John Paulo Edward Waziri alizaliwa miaka 18 iliopita. Mama yake mzazi na John alifariki wakati John ana miaka 3. Baba yake John ndio kalibeba jukumu la kumlea hadi hii leo. Kijana John alifanikiwa kumaliza shule ya msingi na kufaulu kwenda sekondari. Alikwenda kusoma sekondari Kawe Ukwamani ambapo alisoma mpaka kidato cha pili. Hali ngumu ya maisha ndio ilimfanya John kushindwa kuendelea na masomo kwani alipokuwa kidato cha pili John alipata tatizo la moyo ambalo mpaka leo hii linamsababishia uvimbe tumboni kila kukicha. Kutokana na hali duni ya uchumi kwao, John anasumbuka mpaka leo. Kila mwenye afya njema hakosi tabasamu, lakini John amepoteza tabasamu na kukata tamaa ya maisha kutokana na afya yake kuwa mbaya na hali ya uchumu wa familia kuwa mbaya. Ungana na Choice FM 102.5 kupitia MWB – Mji wa Burudani kurudisha tabasamu la John. Tunarudisha tabasamu la John kwa kuchangisha kiasi kisichopungua milioni 4 kwa ajili ya matibabu ya John. Fedha zitakazo patikana zitatumika kurudisha tabasamu la John na atarudi katika hali yake ya kawaida na vile vile ataweza kutimiza ndoto zake.

Zimechangwa: 2,111,901 TZS 42.24%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 180180

Rambirambi Shule ya Lucky Vincent

Rambirambi Shule ya Lucky Vincent

Ndugu watanzania, ukurasa huu ni maalumu kwaajili makusanyo ya rambirambi ya msiba wa wanafunzi (32), walimu (2) na dereva (1) katika ajali iliyotokea Jijini Arusha, katika msafara wa shule yetu ya Lucky Vincent ya Arusha ambapo walikuwa wakienda kufanya mtihani wa kujipima uwezo na wanafunzi wa shule ya Tumaini Junior School iliyopo Karatu. Pesa zote zinapokelewa moja kwa moja na kuratibiwa na uongozi wa shule. Mchango huu kwa sasa utaelekezwa kwa ajili ya rambirambi kwa wafiwa wote na kuratibu shughuli nyingine za mziba. Kwa mawasiliano zaidi: Mr. Jackson Ephraim 0756779097 (Mkuu wa Shule, Lucky Vincent) Mr. Michael Riziki 0768965001 (Mratibu wa Rambirambi) Kwa msaada wa namna ya kutumia mfumo huu wa uchangiaji piga 0752030032.

Zimechangwa: 4,444,031 TZS 8.89%

Zimebaki Siku: 0

Kumb Na: 500500